Mwanaume mwenye umri wa miaka 24 amekamatwa na polisi huko Minna, Jimbo la Niger kwa madai ya kujifanya kama daktari.
–
Mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Clement Joseph ambaye alikamatwa Novemba 6, 2022 pia anadaiwa kuwa na tuhuma kwa kufanya vitendo vya ubakaji ambapo ni kinyume cha sheria dhidi ya wanawake wanne na kumpa ujauzito mmoja wao.
–
Msemaji wa polisi mahala hapo, DSP Wasiu Abiodun, katika taarifa yake alisema mtuhumiwa alikamatwa kwa makosa matatu yakiwamo ya kuiga, kulaghai na kusababisha mimba.
–
“Mshukiwa alikamatwa kwa kujifanya kuwa daktari na kukusanya pesa kwa hila kutoka kwa watu wasio na hatia kwa kisingizio cha uwongo cha biashara feki ya mtandaoni inayoitwa ZUGA COINS” alisema DSP.
–
Alipohojiwa zaidi, mshukiwa alikiri kuwa na ufahamu kwamba vitendo hivyo ni kinyume cha sheria na pia kuna makosa kwa wanawake wanne aliowaingilia bila ya makubaliano pamoja na kumpa mimba mmoja wao.