Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba amekanusha taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa amebadilisha dini na kuwa Muislam.
–
Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Drogba amesema taarifa hiyo sio ya kweli “Hadithi hii inasambaa sana lakini sijabadilisha dini”
–
Ameongezea kusema kuwa “Nilikuwa tu nikitoa heshima kwa ndugu zangu Waislamu niliokuwa nimewatembelea kijijini kwangu, Muda wa umoja, Upendo mwingi na baraka kwa wote”
–
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zimesambaa picha za mchezaji huyo zikionesha akiwa kwenye dua na baadhi ya watu wakidhani kuwa amebadilisha dini na kuwa Muislam.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT