Rais wa Klabu ya Yanga Hersi Said amefunguka kwamba Walikuwa na kikao kilichochukua muda ili kuzungumza na wachezaji wa klabu hio kwamba hakuna wengine wa kuwapatia matokeo hapo Tunisia wakicheza Novemba 9, 2022 dhidi ya Club Africain ya nchini humo bali ni wao wachezaji wenyewe kujituma ndio wanaweza kuipatia klabu hio matokeo mazuri ili kuweza kufuzu kwa hatua zijazo za michuano ya Kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Klabu ya Yanga Mara ya Kwanza ilichezea Nyumbani dhidi ya Klabu hio na kutoka na Sare ya bila kufungana yaani 0-0, kwa sasa wanacho kibarua kipo kwao kukipiga Ugenini.