Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeitaka timu ya Taifa ya Ubelgiji kuondoa neno “Love” kwenye kola ya jezi zao za ugenini.
–
Uamuzi huo wenye unakuja siku mbili kabla ya kikosi hicho cha Roberto Martinez kucheza na Canada, Jumatano jioni,mechi yao ya kwanza katika Kombe la Dunia nchini Qatar.
–
FIFA hawakuwa tayari kwa mazungumzo na walikataa kabisa kujadili suala hilo na Shirikisho la Soka la Ubelgiji. Kwa sasa, Ubeligiji hawajaamua iwapo watakubali ombi la FIFA au laa.
–
Jezi hiyo imekuwa ikiuzwa kwa miezi kadhaa na imeonekana kupendwa na mashabiki, na mpango huo wa neno ‘Love’ kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinasema kuwa haukuwa na uhusiano wowote na kitambaa cha ‘OneLove’ ambacho baadhi ya timu za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ubelgiji, zilitaka kuvaa.
–
Ubelgiji watahitaji jezi mpya zitengenezwe na kutumwa nchini Qatar kutoka kwa kampuni ya Adidas inayotengeneza jezi hizo.