Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar imejivunia haswa kupitia Filamu ya Vuta Nkuvute “Tug Of War” ambayo tarehe 30/10/2022 ilijishindia tuzo nne kati ya 14 ambazo filamu hiyo iliteuliwa kugombea katika hafla iliyofanyika jijini Lagos,Nigeria.
Filamu hiyo ambayo imemshirikisha pia msanii @sitiamina_official ambae pia ni balozi wa Utalii wa Zanzibar katika upande wa sanaa na muziki imeshinda tuzo za 1.Soundtrack bora,
2.Filamu bora katika lugha ya kiafrika
3.Muigizaji mkuu bora na
4.Filamu bora ya mwaka 2022

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT