Kutoka kwenye ukurasa wa mtandao wa Kijamii wa Instagram wa aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga SC, Haji Manara ameandika
–
Katika kuunga Mkono juhudi za Serikali na Rais wetu Kwa kumpa ajira kijana Majaliwa, GSM foundation itatoa Shilingi Milioni Tano ikiwa ni kama Shukran yake Kwa Uokozi mkubwa alioufanya Shujaa huyo mdogo.
–
Mwenyekiti wetu wa Taasisi hii inayojishughulisha na mambo ya kijamii,Ghalib Said Mohammed alinipigia Simu jana jioni kunielekeza nitangaze support yetu Kwa kijana Majaliwa.
–
Mbali na hilo, Rais wa Club ya @Yangasc Eng Hersi Said (@caamil_88 )ambae kwa sasa yupo Tunisia na Team ya Wananchi, akanijulisha kwa njia ya Simu pia , Club ya Yanga itampatia Pikipiki Moja kwa ajili ya Shughuli zake binafsi, tunajua sio jambo kubwa tulilofanya,lakini tunaona ipo haja ya kumfariji Mtu huyu maalum nchini.
–
GSM na Yanga siku zote imekuwa karibu na Jamii, na Kwa kuwa Majaliwa ameokoa roho za Wanajamii wetu,,tumeamua kumtuza ili iwe chachu ya Ujasiri kwa Vijana wengi zaidi nchini.
–
Mbali na Shukran hzo, Mimi na familia yangu pamoja na ‘kuomba Mungu’ kwetu tutampatia The Heroe Majaliwa ,Shilingi milioni moja, binafsi amenifanya nione bado tunao Watanzania ambao ,wapo tayari kuweka rehani roho zao kwa ajili ya kuokoa Binadamu wengine.
–
Ukiacha hilo la kuokoa uhai wa nguvu kazi ya Taifa, Majaliwa ameokoa mamilioni ya Shilingi,ambazo bila shaka yoyote Makampuni ya Bima yangewajibika kulipa iwapo umauti ungewafikia Watanzania wenzetu, kiukweli anastahili kutuzwa
–
Na pia nichukue fursa hii, kutoa wito Kwa Taasisi na Watu binafsi ,wampe moyo zaidi kijana Majaliwa Kwa kumpa walau mkono wa pongezi, hii itakuwa chachu kubwa ya kutengeneza Mashujaa wengi zaidi mfano wa Bwana mdogo huyo, aliyesuuza Mioyo ya Watanzania wengi zaidi, hususan kwenye kipindi hiki cha Majonzi makubwa.