Kwa mujibu wa mrejeo wa historia ya hapo awali juu ya Michuano ya Fainali za Kombe la Dunia tangu kuanzishwa kwake chini ya FIFA, Taifa mwenyeji halijawahi kupoteza mechi yake ya ufunguzi ya Kombe la Dunia.
Lakini kwa sasa historia hio imevurugwa kwa kuwa Qatar ndio nchi ya Kwanza ikiwa ni mweneji wa Maandalizi ya Michuano ya kombe hilo akipoteza akiwa katika Ardhi ya Nyumbani tangu kuanzishwa kwa Kombe la Dunia mnamo miaka ya 1930s.
Mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia 2022 iliwakutanisha Qatar dhidi ya Ecuador kwenye Uwanja wa Al Bayt Nchini Qatar ambapo, Qatar akiwa ndio mwenyeji wa michuano hio amepoteza katika mchezo wao dhidi ya Ecuador kwa goli 0-2 :FT na kutengeneza historia mpya katika soka yaani taifa hilo limekuwa ndio la kwanza kupoteza katika mechi ya ufunguzi wakati ikisalia kuwa ndio mwenyeji wa michuano ya Fainali za Kombe la Dunia.