Msanii H. Baba amedai kitendo cha Harmonize kumchagua Kajala kuwa Meneja wake ni matokeo ya kumuiga Wizkid ambaye mke wake, Jada P ndiye Meneja wake.
–
H. Baba amesema Meneja na mahusiano ni vitu viwili tofauti, huwezi kuvichanganya na kupata matokeo mazuri na pengine ndio sababu ya baadhi ya wasanii kuondoka Konde Music.
“Wanataka kuiga kwa Wizkid, hawawezi. Meneja au mke wa Wizkid alikuwa anamsimamia Chris Brown, kwa hiyo kuja kumsimamia Wizkid ni jambo jepesi kwa sababu ana uzoefu, sasa huyu dada yetu hana uzoefu wa hicho” amesema H. Baba.
–
Utakumbuka tangu Kajala Masanja amekuwa Meneja wa Konde Music, wasanii watatu, Cheed, Killy na Anjella wameachana na lebo hiyo.