Klabu ya Azam FC imetangaza kuwa kuanzia sasa mechi zao zote zilizobaki za msimu huu, watakazocheza katika uwanja wao wa nyumabani Azam Complex, Chamazi hakutakuwa na kiingilio zaidi ya shabiki atatakiwa kuvaa jezi yoyote ya Azam FC.
–
Siku ya Jumatano, Azam FC watashuka dimbani katika dimba la Azam Complex kuvaana na Dodoma Jiji FC katika mechi za muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC, kuanzia Saa 1:00 Usiku.