Klabu ya Southampton imethibitisha kuachana na kocha Ralph Hasenhüttl baada ya jana kupokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Newcastle.
–
Hasenhüttl (55) aliteuliwa rasmi katika klabu hiyo Disemba 6, 2018 na ameiongoza katika mechi 173, akipata ushindi mechi 60, akitoa sare mechi 38 na kupoteza mechi 75.
–
Kwa mujibu wa taarifa ya Southampton, Rubén Sellés atakuwa kocha wa muda na atasimamia mchezo wa Jumatano kabla klabu kutangaza kocha mkuu mpya.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT