Mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani, Miroslav Klose ndiye mchezaji mwenye historia kubwa katika Michuano ya Kombe la Dunia, ameshiriki katika michuano hiyo mara nne (2002, 2006, 2010 na 2014).
–
Klose ameweka rekodi nyingi zinazoendelea kudumu mpaka katika michuano hiyo, akiwa ndiyo Mfungaji Bora wa muda wote katika historia ya Kombe la Dunia akifunga jumla ya mabao 16.
–
Ndiye mchezaji pekee aliyecheza Nusu Fainali nne mfululizo (2002, 2006, 2010 na 2014), ni miongoni mwa wachezaji watatu pekee, walioifunga angalau mabao 5 (2002 mabao 5 na 2006 mabao 5).
–
Pia ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao matatu ‘Hat-trick’ mabao yote matatu akifunga kwa kichwa ilikuwa tarehe 01, 06, 2002 katika mchezo dhidi ya Saudi Arabia ambao Ujerumani ilishinda kwa jumla ya mabao 8-0.
–
Mchezaji pekee aliyefunga mabao mengi kwa kichwa katika Michuano hiyo ya Kombe la Dunia akiwa amefunga jumla ya mabao 5 mwaka 2002)
–
Katika Kombe la Dunia, Miroslav Klose amecheza jumla ya Mechi 24, akifunga jumla ya mabao 16 na kutoa assist 5.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT