
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea kituo ambacho ni miongoni mwa Vituo vilivyoandaliwa kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na ambukizi katika Mkoa wa Dar Es Salaam, amesema yafuatayo;
“Leo nimetembelea Mkoa wa Dares salaam kuangalia utayari wa kukabiliana na wagonjwa wa Ebola endapo tutapata wagonjwa hao.
Nimeridhishwa na kiwango cha maandalizi yaloyofanywa na mkoa chini ya Uongozi wa
Mhe Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa na mratibu wake mkuu, Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Dr Rashid
Hata hivyo bado tunahitaji kuongeza nguvu ktk baadhi maeneo hususani ya kutoa mafunzo kwa Tumu za Haraka za Dharura za kukabiliana na ugonjwa huu, kuongeza Vifaa Kinga na pia kutoa Elimu kwa Wananchi kuhusu dalili za ugobjwa huu na njia za kujikinga
Ninatoa wito kwa Wadau wetu wa maendeleo kutuunga mkono ili kuweza kujiandaa vyema na kukabiliana na Ebola endapo itaingia nchini”.
@wizara_afyatz #zuiaebolatanzania #StopEbolaTanzania




ADVERTISEMENT