Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi kuwa hakutakuwa na ‘Vita Baridi vipya’ na China, baada ya mkutano wa maridhiano na Rais wa China Xi Jinping.
Aliongeza kwa kusema kuwa haamini kwamba China ingeivamia Taiwan.
Mkutano huo ulikuwa wa kwanza kwa viongozi hao wawili wenye nguvu kubwa kuonana ana kwa ana tangu Bw Biden achukue wadhifa huo.
Wawili hao pia waligusia kuhusu uvamizi wa Korea Kaskazini na Urusi dhidi ya Ukraine katika mazungumzo hayo mjini Bali, siku moja kabla ya mkutano wa G20 kwenye kisiwa cha Indonesia.
Source; BBC SWAHILI
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT