
Kamati ya kudumu ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Selemani Kakoso (Mb.) Jumatatu, tarehe 14 Novemba, 2022, imefanya ziara katika Ofisi Kuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jijini Dar es salaam.
Kamati hio ilipokelewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb.) akiambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari; ambapo wataalam wa Mawasiliano wa WHMTH na TCRA walishiriki katika kikao cha pamoja kilichoketi kwa lengo la kufahamu shughuli mbalimbali za Sekta ya mawasiliano ikiwemo utoaji na usimamizi wa Leseni za Mawasiliano.


ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT