Klabu ya Yanga ikielekea kuchuana vikali na Klabu ya Ihefu FC kutokea Mkoani Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Kocha Msaidizi, Cedric Kaze na Captain Bakari Nondo Mwamnyeto wakiwa katika kutazama Dimba litakalotumika kuchezea mechi hio, Highland Estate wafunguka kuhusiana na matarajio yao ya kufikisha Unbeten ya 50 kwa Klabu hio ili kuendeleza historia hio wanaoishikilia kwa sasa hapa Nchini kama Klabu pekee katika Kinyanganyilo hicho.
Kaze akishirikiana na Kocha Mkuu wa klabu hio, Nabi wamekuwa na wakati mzuri kuanzia msimu uliopita kama makocha ambao tangu waungane wameweza tengeneza aina hio ya historia kwa Yanga SC ambayo hakuna Klabu Nyingine imeweza fikisha idadi hio ya Unbeaten katika Ligi kuu mbalimbali zilikwishafanyika hapo awali.