Staa wa muziki wa Marekani, Kelly Rowland anasema ni muda sasa umma umtendee haki nyota wa RnB na Pop, Chris Brown ikiwa ni pamoja na kumsamehe kwa kitendo cha kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki na mfanyabiashara bilionea Rihanna, miaka 14 iliyopita.
–
Katika video ya TMZ, mwimbaji huyo wa ‘Destiny’s Child’ aliulizwa kuhusu wakati wake katika Tuzo za Muziki za Marekani (AMAs 2022), ambapo alikemea vikali umati wa watu waliokuwa wakizomea baada ya jina la Chris Brown kutajwa kama mshindi wa tuzo hizo katika kipengele cha Msanii pendwa wa RnB.
–
Kelly ameongeza na kusema kila mtu anastahili nafasi ya pili, na kwamba sote tunahitaji kipimo cha unyenyekevu… hasa katikati ya makosa yetu wenyewe. Kimsingi, ni jambo la kibanaadamu alilokuwa akilitetea.
–
Hitmaker huyo pia anapendekeza watu wanapaswa kufurahiya mema, badala ya kung’ang’ania mabaya kwa kurusha maneno kila kona hasa inapohusiana na matukio ya karibu miaka 14, kama tukio la Chris na Rihanna.
–
Mwishowe, Kelly anadhani binadamu wote ni wakosefu kwa namna moja au nyingine na wote wanastahili kuanza upya pindi wanapokosea, na kwamba hivyo ndivyo kuwa binadamu.