Mhamasishaji wa Mitandaoni mwenye asili ya kimaasai aliyejizolea umaarufu mkukwa nchini India kutokea hapa nchini, Killy Paul (Maasai Mjanja Duniani) baada ya Kuwavutia wengi kwa jinsi anavyoigiza kucheza na kuimba nyimbo zenye maudhui ya Kihindi, hivi karibuni anatarajiwa kutokea katika moja ya Tamthilia nzuri ifahamikayo kama Jua kali inayorushwa katika Channel ya Maisha Magic Bongo kupitia Kisimbuzi cha Dstv (Multichoice Tanzania.
Hio imedhihirishwa kupitia kurasa za mtandao wa kijamii wa Intagram wa Dstv Tanzaznia kwa kuonyesha kipande kidogo kama kionjo cha ujio wa Killy Paul kupitia Tamthilia hio ya Jua Kali;
@dstvtanzania *Kili Paul ndani ya Jua Kali*“………..Ikiwa hujalipia kifurushi chako , lipia mapema na ufuatilie tamthilia hii yenye kusisimua ya Jua Kali kila siku za Jumatano – Jumapili saa 3:30 usiku kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo 160, ndani ya DStv pekee!
@kili_paul
Huu ndio muonekano wa Killy Paul akiwa katika vazi asilozoeleka kuonekana akilivaa.