
Klabu ya Manchester United imetangaza kuachana na staa wake Cristiano Ronaldo kwa makubaliano ya pande zote mbili.
–
Klabu hiyo imemshukuru kwa mchango wake katika timu hiyo. “Klabu inamshukuru (Cristiano Ronaldo) kwa mchango wake mkubwa katika misimu miwili Old Trafford.” sehemu ya taarifa ya United.
–
Taarifa rasmi ya Cristiano Ronaldo: “Baada ya mazungumzo na Manchester United, tulikubaliana pande zote mbili kumaliza mkataba wetu. Naipenda Manchester United na ninawapenda mashabiki, hilo halitabadilika kamwe.., ninahisi kama ni wakati sahihi wa kutafuta changamoto mpya na ninawatakia kila la kheri Man Utd.”
–
Utakumbuka hivi Karibuni uongozi wa United ulisema unafanyia uchunguzi maneno aliyoyasema staa huyo kwenye mahojiano na mwandishi Piers Morgan.
–
Ronaldo tangu ajiunge kwa mara ya pili Manchester United amecheza mechi 54, mabao 27 akitoa asisti 5.