Wamiliki wa klabu ya Manchester United familia ya Glazers wamekubali kuuza klabu hiyo.
–
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo wameeleza kuwa katika mpango huo wa kuiuza timu watazingatia uwekezaji kwenye kuboresha baadhi ya maeneo ikiwemo uboreshaji wa uwanja na miundo mbinu mingine.
–
Inadaiwa kuwa haya yote yanakuja baada ya mahojiano ya Cristiano Ronaldo baada ya kusema kuwa wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazers hawaijali timu wanachoangalia ni pesa tu.
–
Klabu hiyo imekuwa chini wa familia ya Glazer kutoka Marekani kwa takribani miaka 17 na sasa wameamua kuipiga bei.