Maafisa wa Qatar wamefanya mabadiliko ya ghafla na kuamua kwamba vinywaji pekee ambavyo vitauzwa kwa mashabiki katika viwanja vya michezo wakati wa Kombe la Dunia la mwezi mmoja vitakuwa visivyo vya kileo.
–
Kwa miezi kadhaa FIFA imekuwa ikivutana na Qatar, Taifa la Kiislamu la kihafidhina ambapo uuzaji wa pombe unadhibitiwa vikali.
–
Hatua hiyo imekuwa kizungumkuti kati ya FIFA na kampuni ya pombe ya Budweiser iliyoingia nayo mkataba wa udhamini wa dola bilioni 75.
–
Sambamba na hilo vikwazo hivyo vimewaghadhabisha mashabiki huku waandaaji wakikumbwa na kizaa zaa kufanyia marekebisho zikiwa zimesalia saa 48 kabla ya mchezo wa ufunguzi siku ya Jumapili.
–
Hata hivyo inaelezwa kuwa FIFA ambayo imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji kutokana na uamuzi wa kupeleka mashindano hayo nchini Qatar, huenda ikakosa udhibiti kamili wa maamuzi makubwa kuhusiana na hafla hiyo.
–
Mwongozo rasmi wa FIFA kwa mashabiki unabainisha kuwa wenye tiketi wataruhusiwa kutumia bidhaa za Budweiser, Budweiser Zero, na Coca-Cola ndani ya eneo la uwanja kwa walau saa tatu kabla ya mchezo, na kwa saa moja baadaye.