Timu ya Taifa ya nchini Brazil ndio timu pekee yenye rekodi nzuri katika historia ya soka Ulimwenguni kwa kuchukua jumla ya makombe 5 ya Fainali za michua ya Kombe la Dunia yaliyoandaliwa chini ya FIFA.
Umiliki wa makombe 5 ya Dunia unaipa klabu hio heshima kubwa sana, kiasi kwamba hata Timu nyingine za Taifa zikipangwa nayo huwa na hofu ya kupoteza mchezo.
Katika Michuano ya Fainali ya Kombe la Dunia inayofanyika nchini Qatar, Brazil amekutana na Timu ya Taifa ya nchini Serbia ambapo katika kipindi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana 0-0 HF lakini baada ya kurejea kipindi cha pili Brazil ilibadilisha kabisa hali ya mchezo na kufunga goli 2-0 FT (yaliyofungwa na Richarlison Andrade).
Aina ya chezo ulivyokuwa kipindi cha pili (ni Pira Biriani), umewapa hamasa kubwa mashabiki wa timu ya Brazil kuona ushindi wa Michuano hii upo hivyo wanaona kama wapewe kabisa Kombe hilo mapema.
Ndio maana, mashabiki wa Timu ya Taifa ya Brazil wamejivunia kwa ushindi huo mzuri walioupata dhidi ya Serbia kiasi kwamba kupitia Comments zao katika kurasa mbalimbali za mitandaoni wanaona huu ni wasaa wa kutwaa ubingwa huu kwa mara nyingine na kuweza kufikisha jumla ya makombe 6 katika akiba yao ya rekodi Makombe ya Dunia.