Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amelithibitishia Mwanaspoti kwamba anaondoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo kwa muda akapige shule kidogo.
–
“Nilishaongea na viongozi kila kitu kuhusu kozi hii, naamini watakuwa wanalifanyia kazi suala hilo, Simba ni klabu kubwa itaweka sawa kila kitu, zaidi ya hayo yote namshukuru Mungu kupata fursa hiyo na uzuri nitakuwa narejea kwenye klabu yangu kufanya mafunzo ya vitendo.” alisema Matola.
–
Matola ambaye ana leseni B ya ukocha anakwenda kusoma kozi nyingine ya leseni A ya CAF nje ya Jiji Dar es Salaam ambapo atashindwa kufanya majukumu mawili kwa wakati mmoja.
–
Credit ; Mwanaspoti