Mchezaji katika Safu ya Ushambuliaji Jezi nambari 9 anayekipiga mnamo klabu ya Yanga, Fiston Kalala Mayele ameonyesha maajabu yake tena kwa kufunga goli 3 (Hattrick) katika mchezo wao dhidi ya Singida Big Stars FC uliochezwa Novemba 17,2022 katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Baada ya mechi kutamatika Klabu hio ilitoka na ushindi wa jumla ya mabao 4-1, ambapo goli la nne lilifungwa na mlinzi wa Klabu hio Kibwana Shomari huku kwa upande wa klabu pinzani goli lilifungwa na Medie Kagere (MK 14, Terminator)>Â
“Namshukuru Mungu kwa kufunga Hattrick yangu ya kwanza kwenye Ligi Kuu” Fiston Mayele afunguka hayo baada ya mchezo wao dhidi ya Singida Big Stars.