ADVERTISEMENT
Moja ya Wabunge hapa nchini, Neema Lugangira ambaye alikuwepo miongoni mwa Abiria katika Safari ya Ndege ya Shirika la Air Tanzania hapo jana kuelekea Bukoba Novemba 17,2022 amempogeza Captain na Officer wa Ndege ya Shirika hio kwa maamuzi sahihi waliyoyachukua ili Kujiepusha na ajali kwa kuirejesha Ndege kutua Airport ya Jijini Mwanza. Amefunguka kama ifuatavyo;
@neemalugangira “Abiria wengine wamebaki Mwanza, wengine tumerudi Dar salama. Airport ya Bukoba inajulikana kama airport yenye changamoto kijiographia na hali ya hewa ikiwa mbaya changamoto ya kutua inazidi. Nawapongeza Captain Emmanuel Msangi na 1st Officer Mhayyar Alnabhany kwa maamuzi sahihi”.
“Still shaken lakini Mungu ni Mwema. Nimepanda ndege asubuhi ya leo kwenda Bukoba. Safari ilikuwa na changamoto, tumefika lakini ndege ikashindwa kutua. Nampongeza Rubani kwa uamuzi sahihi wa kurudi Mwanza na sasa narudi Dar. Serikali ibebe kwa uzito suala la airport mpya Bukoba”.
ADVERTISEMENT