
Miili ya watumishi saba wa idara ya afya na elimu waliopata ajali ya gari katika eneo la pori kwa pori katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara imeagwa leo
Wafanyakazi waliofariki katika ajali hiyo ni Joseph Bizuru Thomas,muuguzi, Agapiti Kimario Clemence, Mwalimu, Selina Andrea Nyimbo Mteknolojia, Nickson Damian Mhomwa,tabibu, Catherine Asenga Mhanga muuguzi, Kididi Saidi Athumani, muuguzi na Edward Edwin Makundi daktari.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi.Karolina Mthapula ameongoza kuaga miili hiyo ambapo amesema pamoja na janga lililotokea serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma stahili za afya na elimu
Nao baadhi ha viongozi akiwemo mwakilishi toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Subisya Kabuje, Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi ametoa pole za dhati kwa uongozi wa wilaya ya Kiteto huku baadhi ya viongozi wakitoa salama za pole kwa ndugu wa marehemu na watumishi wenzao
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT