Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.David Sillinde amewaagiza Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuanza mara moja mchakato wa kuweka mipaka halisi kwenye ardhi ambayo ilikuwa na mgogoro baina ya wananchi na Serikali ili watu wasiweze kuvamia eneo hilo.
Mheshimiwa Silinde amesema hayo mnamo tarehe 02 Novemba Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dorothy Kilape Mbunge wa Temeke aliyetaka kujua hatua ambazo Serikali imezichukua baina ya wananchi wanaodai fidia kupisha ujenzi na upanuzi wa Shule ya msingi Uwanja wa ndege katika Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
“Mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na Serikali ilikupisha ujenzi na upanuzi wa Shule ya msingi Uwanja wa ndege ambao ulihitimishwa terehe 26 Septemba 2022 baada ya Mahakama ya Rufaa kutupilia mbali shauri la rufaa namba 116 la mwaka 2019 lililofunguliwa na walalamikiaji 56 ambao walishindwa kuthibitisha madai yao” amefafanua Mhe. Sillinde.


ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT