Mcheaji mahiri mwenye asilili ya nchini Zambia ambaye kwa sasa anakipiga mnamo klabu ya Simba, Moses Phiri (Jenerali) ameirejesha timu yake kukaimu nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara ikiwa imefikisha jumla ya pointi 24 katika michezo 10 baada ya Kuipatia klabu hio Goli moja la kipekee ndani ya kipindi cha kwanza alipopata Assist nzuri kutoka kwa Mohamed Hussein Zimbwe ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo huo uliochezwa ndani ya Dimba la Mkapa yaani FT; Simba SC 1-0 Namungo FC (Southern Killers). Klabu ya Azam FC ndiye kinara anayeishikilia nafasi ya kwanza akiwa na jumla ya pointi 26.