ADVERTISEMENT
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametumia ukurasa wake wa Twitter kukosoa msimamo wa mataifa ya ulaya kuhusu uchafuzi wa hewa na kusema wamekuwa “vigeugeu”.
–
Kupitia ukurasa huo, Museveni ameonesha kusikitishwa na hatua ya Ujerumani kusitisha shamba la umeme wa jua na kuanza uchimbaji wa makaa ya mawe hatua ambayo Museveni amesema ni dhihaka kwa ahadi ya mataifa ya ulaya ya kupambamba na uharibifu wa mazingira.
–
Kutokana na uhaba wa nishati unaoikabili dunia kwa sasa nchi nyingi za ulaya zimeamua kuongeza uzalishaji wa makaa ya mawe hatua ambayo imepingwa vikali na wanaharakati wa mazingira.
ADVERTISEMENT