Mwanaume mmoja kutokea Iran ambaye aliishi katika uwanja wa ndege jijini Paris kwa miaka 18 amefariki dunia.
–
Mehran Karimi Nasseri (77) alijikuta katikati ya utata wa kidiplomasia mwaka 1988 na kuamua kuifanya sehemu ndogo ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle kuwa makazi yake.
–
Mnamo mwaka 1999 alikubaliwa kuwa mkimbizi na kupewa ruhusa ya kuishi nchini Ufaransa , hata hivyo alimua kuendelea kuishi uwanjani hapo hadi mwaka 2006.
Wiki chache zilizopita alirudi katika uwanja huo wa ndege ambapo aliishi mpaka alipofariki kwa sababu za asili.
–
Mr.Nasseri alizaliwa Iran na aliishi miaka kadhaa nchini Ubelgiji baada ya kufukuzwa kutoka nchi kama Uingereza, Uholanzi na Ujerumani kwa kutokuwa na vibali vya uhamiaji. Baadaye alihamia Ufaransa na kuanza maisha yake katika uwanja wa ndege.
–
Hadithi ya maisha ya Mr. Nasseri iliwavutia waandishi wengi na ilimfikia mtayarishaji maarufu wa filamu za Hollywood Stephen Spielberg ambaye aliamua kuandaa filamu ya “The Terminal” ambayo ilichezwa na waigizaji maarufu Tom Hanks na Catherine Zeta-Jones. Filamu hiyo ilitoka mwaka 2004.