Ligi kuu ya Tanzania Bara imeendelea kukua kwa kasi na kushika hatamu kimataifa zaidi kwani wadau wa soka wameanza kuwa karibu zaidi kwa kufuatilia soka linalochezwa hapa nchini wakitoka mataifa mengineyo. Hio imejidhihirisha kupitia wadau wawili @loulou_hassan na @rashidyabdalla kutoka @citizentvkenya waliohudhuria na kushuhudia soka biriani katika dimba la Azam Complex. Ligi kuu ikiwa chini ya Udhamini mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara kwa kushirikiana na Chombo cha habari AZAM TV katika upande wa kurusha matangazo ya mechi zote za ligi hio imeleta chachu Kwa wadau kutokea nje kupenda kusapoti soka la Tanzania Bara, Afrika Mashariki na kutoa hamasa ya kuona Mchezo wa mpira wa miguu utakuwa moja ya michezo inayoaminika na kuingiza pato kubwa la taifa kupitia mahusiano ya karibu yanayojengeka na mashabiki wahuzuriao kushuhudia mitanange kadha wa kadha itakayochezwa nchini Tanzania.