Nguli wa soka Duniani na mtambo wa zamani wa mabao wa Brazil, PELE amempongeza mshambuliaji wa USA
, Timothy Weah kufuatia goli lake dhidi ya Wales.

–
“Lilikuwa bao maridadi, Endelea kutimiza ndoto zako, ndoto huwa kweli” amesema Pele.
–
“Ahsante Papa Pele, Ni baraka na heshima kupokea ujumbe huu wa kutia kutoka kwa mfalme mwenyewe. Ahsante kwa kila kitu ulichokifanya kwa ajili Ulimwengu na kwa ajili yetu vijana weusi” Timothy Weah alimjibu Pele.
–
JE WAJUA:
Timothy Weah na Pele ndio wachezaji pekee kuwahi kufunga goli dhidi ya Wales kwenye kombe la Dunia.
–
Timothy Weah ambaye ni mtoto wa Rais wa sasa wa Liberia, George Weah aliifungia Marekani bao katika sare ya 1-1 dhidi ya Wales katika mchezo wa kundi B wa kombe la Dunia 2022.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT