Kupitia Kurasa za mitandao ya kijamii, Shirika la Ndege lifahamikalo kama Precision Air limetoa taarifa inayokanusha Uvumi unaendelea mitandaoni kuhusiana na taarifa ya Ndege ya Shirika hilo kutajwa katika tukio la kushidwa kutua Mjini Bukoba na kurejea katika Airport ya jijini Mwanza kutokana na hali nzuri ya kijiografia, ikisema taarifa hizo sio za kweli na zipuuzwe kwanza kwa siku ya Jana Novemba 17,2022 hapakuwa na ratiba ya Ndege kutoka Shirika hilo kuruka kuelekea huko.
Lakini ukweli uliopo ni kwamba ndege iliyohusika na Tukio hilo ni ya Shirika la Air Tanzania ambapo baadhi ya Wateja wake walisalia Mwanza baada ya Ndege kurudi kutoka Bukoba na wengine Wakirejea jijini Dar es Salaam.