Rais wa FIFA, Gianni Infantino ametoa wito wa kusitishwa kwa vita kati ya Ukraine na Urusi wakati wa Kombe la Dunia la FIFA.
–
Mgogoro kati ya Urusi na Ukraine umeendelea kwa muda mrefu sasa, huku Warusi wakiwa tayari wamepigwa marufuku kushiriki Kombe lijalo la Dunia nchini Qatar.
–
Wakati mzozo ukiendelea, Infantino amehimiza kusitishwa kwa mapigano wakati wa mashindano hayo.
–
Rais wa FIFA alikuwepo wakati wa chakula cha mchana jana Jumanne kilichohusisha viongozi wa mataifa makubwa ya kiuchumi ya G20 na wakati huo, alitoa wito kwa nchi hizo mbili kuleta usitishaji wa muda wa mapigano na kutumia Kombe la Dunia kama ‘sehemu ya kudumisha amani’
–
“Ombi langu, mfikirie juu ya usitishaji vita kwa muda wa mwezi mmoja, kwa muda wote wa Kombe la Dunia” alisema
–
Infantino alisisitiza kwamba Soka linaweza kutumika kama njia ya kuleta amani duniani, kwa matumaini kwamba michuano hiyo inaweza kuwa kichocheo cha sehemu ya amani kwa Ukraine na Urusi.
–
Mchezo wa kwanza wa Kombe la Dunia utawakutanisha Qatar dhidi ya Ecuador siku ya Jumapili.