Mshambuliaji wa Klabu ya Man United na Timu ya Taifa ya England, Marcus Rashford amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi kati ya England na Wales.
Rashford ndiye aliyefunga magoli mawili katika ushindi wa 3-0 wa England dhidi ya mpinzani wake Wales katika dimba la Ahmed Bin Ali, Qatar.
Bao lingine la England liliwekwa kimiani na kiungo Phil Foden. England imetinga hatua ya 16 bora ambapo itachuana na Wawakilishi wa Afrika Senegal katika hatua hiyo ijayo.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT