Mmiliki wa mtandao wa Twitter Elon Musk amesema kuwa aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amerejeshewa akaunti yake ya twitter.
–
Mtandao huo uliendesha kura ya maoni ya kutaka kujua endapo Trump arejeshewe akaunti hiyo au la.
–
Musk, tajiri namba moja duniani amesema asilimia 51.8 ya watumiaji milioni 15 wa Twitter wametaka akaunti ya Trump ifunguliwe.
–
Hata hivyo, huenda Trump asiutumie tena mtandao huo. ”Sioni sababu ya kufanya hivyo,” amenukuliwa Trump akisema.
–
Akaunti yake ilifungiwa mwaka 2021 kwa maneno yake ya uchochezi.
–
Utawala wa zamani wa Twitter kabla ya Musk kuununua, uliifunga akaunti hiyo ya Trump baada ya waandamanaji kuandamana mjini Washington DC kwa maneno yake ya kuudhi.
–
Lakini Trump, mmoja wa viongozi matajiri, miezi michache baadae alianzisha mtandao wake unaoitwa ‘Truth Social’.
–
Musk tayari amechukua hatua kadhaa za kile anachokiita kuboresha mtandao huo ikiwemo kupunguza wafanyakazi.