Mwamuzi mtarajiwa wa kombe la Dunia Facundo Tello aliyekuwa akichezesha mchezo wa fainali ya kombe la Washindi Nchini Argentina siku ya Jumapili kati ya Racing Club na Boca Juniors aligawa kadi nyekundu kama njugu katika mchezo ambapo Racing Club ilishinda 2-1 baada ya muda wa ziada.
–
Wakati ubao ukisoma 1-1 katika dakika ya mwisho ya muda wa ziada, kiungo wa Racing, Carlos Alcaraz aliifungia klabu yake bao la pili na kwenda kushangilia mbele ya mashabiki wa Boca Juniors kwa muda mrefu hali iliyowatia hasira wachezaji wa Boca Juniors huku video zikionesha wachezaji hao wakimkamata sikio na kumrushia mpira.
–
Tello ambaye atakuwa mmoja wa Waamuzi wa kombe la Dunia alimlima Alcaraz kadi nyekundu huku akiwatoa wachezaji watano wa Boca Juniors. Kwa ujumla kadi nyekundu tatu zilitoka kwa wachezaji wa Racing Club na saba kwa wachezaji wa Boca Juniors katika mechi hiyo
–
Boca Juniors ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Norberto Briasco kabla ya Matias Rojas wa Racing kusawazisha katika kipindi cha kwanza.