ADVERTISEMENT
Nyota wa zamani wa Bayern Munich na Ufaransa, Frank Ribéry anatarajiwa kurejea katika klabu hiyo ya Bundesliga chini ya jukumu jipya.
–
Ribery (39) anatarajiwa kuwa balozi wa klabu, mazungumzo ya awali tayari yamefanyika kati ya pande zote mbili na yanaendelea vizuri.
–
Ribéry atachukua majukumu ya uwakilishi (Balozi) wa Bayern katika siku zijazo, si mchezaji wa kwanza wa zamani kuchukua nafasi hii huku wachezaji kama vile Giovane Elber (50) na Claudio Pizarro (44) wakiwa tayari wamechukua kazi sawa na klabu.
–
Tangu alipostaafu mwezi Oktoba kutokana na majeraha ya mara kwa mara ya goti, Ribéry amekuwa akifanya kazi kama kocha msaidizi katika klabu ya Serie A, Salernitana ambayo kwa sasa ipo nafasi ya 12.
ADVERTISEMENT