Mchezaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amemjibu mshambulaji wa zamani wa Klabu hiyo Wayne Rooney ambaye alimkosoa siku za hivi karibuni akisema anamuonea wivu.
ADVERTISEMENT
–
Akizungumza alipokuwa anafanya mahojiano na Piers Morgan, Ronaldo alisema: “Sijui kwa nini ananikosoa vibaya labda kwa sababu alimaliza kazi yake na mimi bado naendelea kucheza kwa kiwango cha juu sio hivyo tu hata muonekano nimemzidi kwa sasa.’’
–
ADVERTISEMENT
Ronaldo na Rooney, wote wenye umri wa miaka 37, walifcheza pamoja Man United kati ya 2004 na 2009.