Mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane hatashiriki Kombe la Dunia kutokana na jeraha la mguu alilopata alipokuwa akiichezea Bayern Munich.
–
ADVERTISEMENT
Mchezaji huyo alipata jeraha kwenye mguu wake wa kulia katika ushindi wa 6-1 kati ya Bayern dhidi ya Werder Bremen Jumanne iliyopita.
–
ADVERTISEMENT
Mane alijumuishwa katika kikosi cha wachezaji 26 cha Senegal kwa Kombe la Dunia lakini nyota hatashiriki Qatar baada ya kushindwa kupona jeraha hilo.
–
Kwa mujibu wa habari, Mane alifanyiwa vipimo zaidi kabla ya kuthibitishwa kuwa alihitajika kufanyiwa upasuaji.