ADVERTISEMENT
Serikali imewahakikishia wananchi wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha kuwa hakutakuwa na ongezeko la nauli ya treni inayopita katika mikoa hiyo ili kuwawezesha kufanya safari zao kwa urahisi hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
ADVERTISEMENT
Akizungumza jijini Arusha, baada ya kutembelea Stesheni ya reli ya kati Naibu Waziri Mwakibete amesema kuwa uwepo wa treni hiyo umerahisisha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo baina ya Dar es Salaam na mikoa hiyo na hivyo Serikali inatarajia kuongeza idadi ya mabehewa ili kuwawezesha abiria wengi zaidi kutumia usafiri huo.