
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa pili kulia) amekabidhi tuzo na cheti cha utambuzi kwa uongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi (wa pili kulia) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa Benki ya NBC kufanikisha maendeleo ya sekta ya viwanda nchini katika tuzo za 16 za Rais kwa vinara wa Uzalishaji viwandani (PMAYA) zilizoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI).
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.