Msanii maarufu mwenye asili ya Colombia Shakira anatarajiwa kutumbuiza kwenye ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Dunia 2022 jijini Doha.
–
Wasanii wengine ni pamoja na bendi maarufu ya Hip hop Black Eyed Peas na kundi maarufu kutokea Korea Kusini BTS. Shakira ametajwa kuwa ni Malkia wa Kombe la Dunia kwa upande wa soka hii ikiwa ni mara yake ya nne kutumbuiza.
–
Mara ya kwanza alitumbuiza katika Kombe la Dunia 2006 nchini Ujerumani akiimba nyimbo zake maarufu za ”Hips Don’t Lie” na ” Bamboo” alizomshirikisha Wyclef Jean.
Mwaka 2010 alikuja na wimbo wa ”Waka Waka ”katika Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini na mwaka 2014 alitumbuiza kwenye sherehe za kufunga Kombe la Dunia nchini Brazil na wimbo wake wa ”La la la la la’.
–
Hivi sasa Shakira anatamba kwa nyimbo zake kama ”Monotonia” na ”Te felicito” ambazo zimepokelewa kwa kishindo kikubwa kwenye majukwaa mbalimbali ya kidigitali.
–
Kwa upande mwingine Shakira anaufunga mwaka akiwa amezungukwa na taarifa mbalimbali za talaka yake kutoka kwa nyota wa soka Gerard Pique. Kwa wiki kadhaa sasa taarifa hizo zimekuwa zikitanda kwenye televisheni na mitandao ya kijamii.