ALIYEKUWA kipa wa Mtibwa Sugar, Faruk Shikhalo amekubali yaishe baada ya kusitisha mkataba na klabu hiyo kisha kutimkia kwao Kenya.
–
Hatua hiyo inakuja kufuatia kipa huyo kuwa katika lawama kwa mashabiki na hata baadhi ya viongozi wa klabu hiyo kwa madai ya kuyumba kwa kiwango chake.
–
Akizungumza akiwa kwao Kenya kwa njia ya simu Shikhalo amesema amelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kuona mambo hayaendi sawa.
–
Amesema amechukua uamuzi huo Novemba 14 siku moja baada ya mchezo wa timu hiyo dhidi ya Azam ambao ulimalizika kwa Mtibwa kupokea kipigo cha mabao 4-3.
–
Chanzo : Mwanaspoti