ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, April 1, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji na Uwekezaji (UNCDF) limeteua Benki ya NBC kuwa Mtaalam Mshauri wa kukamilisha Hati Fungani ya Mamlaka ya Maji Tanga

I am Krantz by I am Krantz
Nov 15, 2022
in HABARI
0
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji na Uwekezaji (UNCDF) limeteua Benki ya NBC kuwa Mtaalam Mshauri wa kukamilisha Hati Fungani ya Mamlaka ya Maji Tanga
0
SHARES
45
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

Picha ya pamoja kwenye makabidhiano ya mkataba wa maridhiano,taasisi ya maji safi na taka ya Tanga-UWASA juu ya uanzilishwaji wa hati fungani za kukusanya fedha kwaajili ya kuboresha mfumo wa maji jijini Tanga,kuanzia kushoto ni Mkurugenzi Sera na Mipango-Tamisemi John Cheyo, Mkuu wa UNCDF-Tanzania Peter Malika,Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa benki ya NBC, Bw. James Meitaroni James Meitaron na Mkurugenzi kutoka Tanga-UWASA Geofrey Hill.

 

RelatedPosts

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

Apr 1, 2023

GARI LA KIFAHARI ZAIDI NA LENYE THAMANI KUBWA

Apr 1, 2023

ONYANGO AOMBEWA MSAMAHA KWA ALICHOFANYA

Apr 1, 2023
Load More

 15th November 2022,

Dar es Salaam – Leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji na Uwekezaji (UN Capital Development Fund -UNCDF) limetangaza rasmi uteuzi wa Benki ya NBC kuwa mtaalam mshauri atakayekamilisha hatua za msingi kuwezesha kuuzwa kwa Hati fungani ya Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga UWASA) ambayo itakuwa ya kwanza kuwahi kutolewa na taasisi ya Serikali nchini.

Tangazo hilo la uteuzi limeambatana na utiaji saini wa makubaliano ya kimkakati baina ya UNCDF na Benki ya NBC ambayo itaongoza timu ya wataalamu washauri inayojumuisha taasisi tano zinazotoa huduma za ushauri wa kifedha na uwekezaji na kusajiliwa na Mamlaka ya soko la hisa na mitaji (Capital Market and Securities Authority-CMSA). Hatua hii ya uteuzi ni kwa mujibu wa matakwa na miongozo ya CMSA ambapo timu hiyo inatarajiwa kuhakikisha hati fungani ya Mamlaka ya Maji Tanga inaorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ifikapo robo ya kwanza ya mwaka 2023.

Mkurugenzi wa Tanga UWASA, Bw. Geofrey Hill

Akiongea katika hafla hiyo ya utiaji Saini, Mkurugenzi wa Tanga UWASA, Bw. Geofrey Hill, amesema, “Siku hii muhimu imefikiwa kutokana na ushirikiano wetu na UNCDF na kwa kuzingatia miongozo na maelekezo ya Serikali ya kutafuta vyanzo mbadala vya fedha ili kutekeleza miradi ya maendeleo. Tunatarajia kufanya kazi kwa ukaribu na NBC ili kuharakisha hatua zilizobaki kuwezesha upatikanaji wa fedha zitakazotumika kuboresha na kuongeza uwezo wetu wa kusambaza maji kwa wananchi na maeneo yasiyo na huduma hiyo”.

Kadhalika, akitoa salamu zake Mkuu wa Shirika la UNCDF Tanzania Bw. Peter Malika, alieleza kuwa “Tunajivunia kuwateua NBC ambayo ni taasisi ya kitanzania kukamilisha suala hili la kihistoria.  Hii ni njia mojawapo ya kuimarisha na kujenga uwezo wa ndani (national capacities) kuibua na kutumia vyanzo bunifu vya fedha kugharamia maendeleo. UNCDF kama mdau wa maendeleo ina nafasi muhimu ya kusaidia kutatua changamoto za upatikanaji wa fedha hususani kwenye nchi zinazoendelea ambazo masoko ya fedha ni machanga.”

Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa benki ya NBC, Bw. James Meitaroni alisema “Tukiwa kama Benki ya kizalendo,  tunajivunia kuwa taasisi ya kifedha ya kwanza nchini kushiriki kama kiongozi wa mchakato na mtaalam mshauri, katika kuhakikisha ukamilifu na uuzwaji wa hati fungani hii ambayo itakuwa ni ya kwanza kutokea nchini Tanzania. Leo tumeshuhudia historia ikiandikwa ambapo kwa mara ya kwanza nchini, Mamlaka ya Umma  imefungua milango mipya ya kupata fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Fedha zitakazopatikana kutoka kwenye mauzo ya hati fungani zitaenda moja kwa moja kurekebisha miundombinu ya maji ya mji wa Tanga na hivyo kuongeza tija ya upatikanaji na usambazaji maji jijini Tanga. Tunajivunia kuwa Benki washauri  na kutumia uzoefu wetu katika kuleta suluhu ya changamoto zinazokabili jamii. Kupitia hati fungani hizi tunaenda kupata suluhu kubwa ya tatizo la upungufu wa mji mkoani Tanga na vijiji vya jirani. Tunaishukuru sana serikali na wadau wengine kama UNCDF kwa kuendelea kuweka mazingira bora yanayofanya taasisi za kifedha kama sisi NBC kushiriki katika shughuli za kutatua changamoto za jamii inayotuzunguka”

ADVERTISEMENT

ADVERTISEMENT

MWISHO

Related

I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI
HABARI

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
GARI LA KIFAHARI ZAIDI NA LENYE THAMANI KUBWA
HABARI

GARI LA KIFAHARI ZAIDI NA LENYE THAMANI KUBWA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
ONYANGO AOMBEWA MSAMAHA KWA ALICHOFANYA
HABARI

ONYANGO AOMBEWA MSAMAHA KWA ALICHOFANYA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
KOCHA NABI NA WACHEZAJI HAWA KUKOSA MCHEZO DHIDI YA MAZEMBE, SABABU YATAJWA
HABARI

KOCHA NABI NA WACHEZAJI HAWA KUKOSA MCHEZO DHIDI YA MAZEMBE, SABABU YATAJWA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
TANI 20.6 ZA BANGI ZIMEKAMATWA 2022
HABARI

TANI 20.6 ZA BANGI ZIMEKAMATWA 2022

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
SAFU YA ULINZI IMEWAANGUSHA SIMBA
HABARI

SAFU YA ULINZI IMEWAANGUSHA SIMBA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
November 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930  
« Oct   Dec »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In