Kikosi cha Simba SC kimewasili jijini Mbeya tayari kwa kusubiri kuikabili klabu ya Mbeya City FC katika mchezo wao wa Novemba 23,2022 katika Michuano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Klabu hio ikiwa bado inafuraha ya ushindi wa nyuma uliopatikana baada ya kuipa kichapo kikali Klabu ya Ruvu Shooting FC kwa jumla ya goli 4-0, sasa bado inashauku ya kuwa na muendelezo mzuri kwa kujikusanya Pointi zote 12 katika mechi zote 4 watakazocheza nje yaani katika viwanja vya ugenini ikiwa itaanza na Mbeya City FC kama timu ya kwanza ili hali bado huwawia vigumu kumfunga mpinzani huyo katika misimu mingi wanapokuna nae.