Binti mmoja mkazi wa kijiji cha Mahaha, wilayani Magu, mkoa wa Mwanza, Zawadi Msagaja anayeaminika kuwa na umri wa miaka 20 anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumzika mtoto akiwa hai ili aweze kujipatia mali (utajiri).
Ikiripotiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema watuhumiwa wanadaiwa kutenda unyama huo mnamo Novemba 13 mwaka huu majira ya mchana katika mtaa wa Kisundi, kata ya Bugogwa, wilayani Ilemela.
Aidha wengine wanaohusishwa na kushikiliwa juu ya tuhuma za tukio hilo ni dada yake Zawadi, Elizabeth Kaswa na mumewe, Mussa Mazuri ambaye ni mganga wa kienyeji aliyetoa maagizo ya kutekeleza kitendo hicho huku akimtishia Zawadi kuwa asipofanya hivyo yeye ndiyo atatolewa kafara.
Credit; Mwananchi Scoop