ADVERTISEMENT
TAARIFA: HALI YA HUDUMA YA MAJI JIJI LA MWANZA NA VIUNGA VYAKE NOVEMBA 26, 2022
–
Tumepokea taarifa kutoka TANESCO kwamba Tarehe 26 Novemba, 2022 (Jumamosi) kuanzia Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 10:00 Jioni watazima umeme ili kupisha maboresho ya miundombinu yao na miongoni mwa maeneo yatakayoathirika ni pamoja na eneo la chanzo cha maji (Capripoint).
–
Kwa muda wote huo hakutakuwa na uzalishaji wa maji na hivyo maeneo yote ya Jiji la Mwanza na viunga vyake yataathirika.
–
Tunawasihi kuanzia sasa kuhifadhi maji yatakayotumika wakati wote wa matengenezo ya TANESCO.
–
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza, huduma itarejea katika hali ya kawaida baada ya nishati ya umeme kurudi.
–
Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano MWAUWASA
22/11/2022
Upatapo taarifa hii, tafadhali mfahamishe na mwingine

ADVERTISEMENT