Taarifa ya awali ya ripoti ya ajali ya ndege inayomilikiwa na shirika la Precision iliyotokea katika eneo la Ziwa Victoria Tanzania, imetolewa na wizara ya ujenzi na uchukuzi nchini ambapo katika ripoti hiyo imeonekena kuwa vikosi vya uokoaji vilichelewa kufika katika eneo la tukio kutokana na kwamba utayari wa huduma za dharura kwenye ajali ya Ndege ya Precision Air haukuwa mzuri.
–
Aidha, miongoni mwa mambo mengine yaliyotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na Wazamiaji kushindwa kuanza kazi ya uokoaji mana mitungi yao haikuwa na oksijeni, Kitengo cha Polisi wa majini kuwa na Boti moja na lilifika eneo la tukio masaa manne baadaye, na halikuwa na mafuta ya kutosha.
–
Lakini pia Ripoti hiyo imeeleza kwamba maisha ya wengi zaidi yangeliweza kuokolewa endapo kama huduma za uokoaji zingelifika mapema zaidi.