ADVERTISEMENT
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanwake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amekutana na Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa na timu ya SMAUJATA tarehe 07 Novemba, 2022 ambapo amepokea taarifa kuhusu mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kwa watoto ikiwemo ufuatiliaji wa shauri la ukatili dhidi ya watoto wawili wa familia moja, katika kata ya Kivule.
Mhe. Dkt. Gwajima ameelekeza mkoa ufanye uchunguzi na taarifa iwasilishwe Wizarani. Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwapa semina fupi SMAUJATA kuhusu majukumu yao na jinsi ya kuendelea kuimarisha ufanisi wa kazi zao kama sehemu ya jamii kushirikiana na Serikali kwenye kupiga vita ukatili wa kijinsia na kwa watoto.

ADVERTISEMENT