ADVERTISEMENT

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefanya semina ya matumizi salama ya mtandao na maisha mapya kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT), Mwanza, tarehe 8 Novemba, 2022.
Semina imeratibiwa na ofisi ya TCRA Kanda ya Ziwa chini ya uongozi wa Mhandisi Francis Mihayo na menejimenti ya chuo ambapo mada mbalimbali za uelewa wa masuala ya matumizi salama ya mtandao ziliwasilishwa.
Aidha Chuo hicho kimezishukulu Taasisi zilizoungana nacho katika kufanya Orientation Program kwa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Masomo 2022/2023 kama ifuatavyo;
“Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza Saint Augustine University of Tanzania leo tarehe 8/11/2022 wamehitimisha zoezi la orientation kwa kupokea ujumbe maalum wa kuwakaribisha kwa mwaka wa masomo 2022/2023.
Tunawashukuru sana Tanzania Communications Regulatory Authority kwa elimu waliyoitoa kwa wanafunzi wetu kuhusu “Matumizi Salama ya Mitandao ya Kijamii”.
Tunapenda pia kuwashukuru Tanzania Tourist Board kwa elimu waliyoitoa kwa wanafunzi wetu kuhusu Sekta ya Utalii na Mchango wake kwa Taifa.

Makamu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza, Rev. Costaricky Mahalu akizungumza katika Programu maalumu ya Kuhamasisha Matumizi Salama ya Mtandao.



ADVERTISEMENT